Kwa mujibu wa tovuti ya Detnews, mashirika hayo ya Kiislamu yamemwandikia barua mwendesha mashtaka huyo yakisema kuwa, polisi wa FBI wamekuwa wakiingia katika miskiti na vituo vya utamadui vya Kiislamu kwa lengo la kuwatafuta watu wanaoweza kushirikiana nao katika kupeleleza na kufanya ujasusi kuhusiana na shughuli na itikadi za Waislamu katika vituo hivyo.
Voctor Beg, Mkuu wa Jumuiya za Kiislamu za Michigan ambaye ana jukumu la kusimamia shughuli za misikiti na vituo vya Kiislamu vya eneo hilo amesema kuhusiana na suala hilo kuwa, Waislamu kama walivyo raia wengine wa Marekani, wanataka kuwepo amani na usalama kamili nchini humo na kuilinda nchi hiyo kutokana na tishio lolote, lakini kwamba wanapinga kabisa suala la polisi ya FBI kuingia miongoni mwa Waislamu na kuwataka wawafanyie ujasusi kwa kisingizio cha kulinda usalama wa nchi hiyo.
Katika upande wa pili, mashirika ya kutetea haki za raia nchini Marekani yamekosoa vikali hatua hiyo ya FBI ya kufanya ujasusi kuhusiana na shughuli za Waislamu wa Marekani. Kerry Moose, Mkuu wa Muungano wa Uhuru wa Kiraia nchini Marekani pia amesema kwamba, wakuu wa masuala ya usalama wa Marekani wanapasa kutumia nguvu zao zote kulinda usalama wa nchi hiyo na sio kujishughulisha na ujasusi wa itikadi za kisiasa na kidini za raia wa nchi hiyo. 389702