IQNA

Jumuiya ya ya Nchi za Kiarabu yaitaka jamii ya kimataifa kusimamisha jinai za Israel

14:30 - April 18, 2009
Habari ID: 1766415
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeitaka jamii ya kimataifa hususan Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za kusimamisha jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Mahmoud Rashid harakati za utawala ghasibu wa Israel katika Quds Tukufu na dhidi ya wakazi wa Kiarabu wa eneo hilo zinakiuka sheria za kimataifa.
Mahmoud Rashid ameutaka Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa kukomesha vitendo hivyo vya Israel na kuwalinda wananchi wa Palestina waoishi katika mashaka na manyanyaso tangu miaka sitini iliyopita.
Amesisitiza kwamba Baitul Muqaddas ni mji wa Kiislamu na Kiarabu na kwamba historia na utambulisho wa mji huo hauwezi kutoweka kwa hatua zisizokuwa za kisheria utawala wa Israel.
Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesisitiza kuwa jinai na uchokozi wa Israel huko Baitul Muqaddas zitachunguzwa katika kikao kijacho cha Kamati ya Kudumu ya Haki za Binadamu ya nchi za Kiislamu na Kiarabu. 390012

captcha