Hujjatul Islam Hassan Safinasab ameashiria wito wa kufanya mazungumzo na Iran uliotolewa na Marekani kufuatia mafanikio makubwa ya Tehran katika medani ya nishati ya nyuklia na akasema kuwa Wazayuni walioshindwa na Hizbullah katika vita vya siku 33 huko Lebanon na kupata kipigo huko Gaza, watapata kipigo kikali na kuangamizwa iwapo watafanya makosa ya kuishambulia kijeshi Iran.
Amesema kuwa hatua ya Marekani ya kubadili msimamo wake kuhusu Iran ni dalili ya nafasi madhubuti ya utawala wa Kiislamu hapa nchini na akaongeza kuwa Marekani imebadili msimamo wake kutokana na azma ya taifa na utawala wa Kiislamu ambao umejizatiti kwa moyo wa kupambana na ubeberu wa Mapinduzi ya Kiislamu na muasisi wake hayati Imam Khomeini.
Imam wa Swala ya Ijumaa ya Gunabad amesema utawala haramu wa Israel unazungumzia suala la kusitishwa miradi ya nishati ya nyuklia nchini Iran ilhali wenyewe unamiliki silaha hatari za nyuklia na umekataa kutia saini mkataba wa kuzuia uzalishaji wa silaha hizo hatari duniani na kukaguliwa taasisi zake za nyuklia. 390181