IQNA

Kumalizika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani kwa askari usalama wa Saudi Arabia

8:55 - April 20, 2009
Habari ID: 1767071
Sherehe za kumalizika mashindano ya kwanza ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu maalumu kwa askari usalama na polisi ya Saudi Arabia zimefanyika siku ya Jumapili mjini Riadh, mji mkuu wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la mtandano la nchi hiyo la al-Iqtisadiya, sherehe hizo zimesimamiwa na Amir Naif bin Abdul Aziz, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia na makamu wake Amir Muhammad bin Naif bin Abdul Aziz. Aidh al-Qarani, Mkuu wa Idara ya Mwongozo na Uhubiri wa Kiislamu ya nchi hiyo amesema kuwa lengo la kufanyika mashindano hayo lilikuwa ni kushajiisha na kuwahamasisha askari usalama na polisi ya nchi hiyo kuhifadhi Qur'ani Tukufu pamoja na kutekeleza mafundisho yake na kuleta mfungamano baina ya mafundisho na vitendo.
al-Qarani amesema kuwa watu 350 walishiriki katika mashindano hayo, ambapo 65 kati yao walifanikiwa kufikia hatua ya mwisho ya mashindano hayo. Amesema washindi 15 kati ya hao watapewa zaidi nono ya riali laki moja na nusu za Saudia.
Mashindano hayo yamefanyika katika hatua tano ambazo ni kuhifadhi juzuu 15, juzuu 10, juzuu 5, juzuu 3 na hatimaye juzuu moja ya kitabu kitakatifu cha Qur'ani. 390821
captcha