Mkutano huo uliotayarishwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Toronto utahudhuriwa na wasomi na wanafikra wa Kiislamu kutoka nchi za Misri, Saudi Arabia, Malaysia, India, Syria na Pakistan.
Baadhi ya masuala yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na masuala ya fedha na masharti ya bima, namna ya kuainisha nyakati za swala, zaka na matumizi yake sahihi na kiwango cha kushiriki Waislamu katika harakati mbalimbali za kisiasa. 390981