Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa katika kipindi cha sasa Tehran ina uhusiano na serikali ya Cairo na daima imekuwa ikiwausia viongozi wa Misri kutilia maanani maslahi ya ulimwengu wa Kiislamu na vitisho vinavyotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel na viongozi wenye misimamo ya kupindukia mipaka wa utawala huo dhidi ya Waislamu.
Hassan Qashqavi ameyasema hayo kufuatia tangazo lililotolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwamba jumuiya hiyo iko tayari kuwa mpatanishi kati ya Iran na Misri.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza juu ya umuhimu wauamoja na mshikamano wa Kiislamu na akaongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inakaribisha hatua yoyote ya kuimarisha umoja na mshikamano kati ya nchi za Kiislamu ikiwemo Misri.
Kuhusu hotuba ya Rais wa Iran katika mkutano wa kimataifa wa kupiga vita ubaguzi mjini Geneva, Qashqavi amesema kuwa hotuba hiyo iliwakilisha sauti ya fikra za waliowengi duniani dhidi ya ubaguzi na ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 391451