Ameyasema hayo katika mkutano wa Waendesha Mashtaka wa nchi za Kiislamu na wanasheria wa kimataifa uliomalizika jana mjini Tehran na kuongeza kuwa kufanyika kwa mkutano huo na kiwango cha nchi za Kiislamu zilizoshiriki kunaonyesha kwamba nchi hizo zinatoa kipaumbele kwa suala la kutekelezwa uadilifu na kwamba hakuna jambo lolote linaloweza kuzizuia nchi hizo kutekeleza majukumu yao.
Amin Khatib amesema kuwa utawala ghasibu wa Israel umezidisha harakati za kuvuruga amani katika Mashariki ya Kati na akasisitiza juu ya kuchukuliwa hatua za kisheria za kuwashughulikia watenda jinai wa utawala huo.
Mwanasheria huyo mkongwe ameashiria kimya cha jumuiya za kimataifa mbele ya jinai za Israel huko Palestina na akasema kuwa kutegemea jumuiya za kimataifa kwa ajili ya kutekelezwa sheria na uadilifu hakuna maana yoyote kwani hadi sasa jumuiya hizo hazijachukua hatua yoyote ya maana ya kuwatetea wananchi wa Palestina.
Amin Khatib amezitaka nchi za Kiislamu kudhihirisha uwezo wao kwa walimwengu kwa kutegemea umoja na mshikamano wa Kiislamu. Mwanasheria huyo wa Kilebanon amelaani utumiaji wa silaha zilizopigwa marufuku katika mashambulizi ya Israel dhidi ya wananchi wa Gaza na akasema watu wengi na vyombo vya habari vinazungumzia suala la kutumiwa silaha za fosforasi nyeupe katika mashambulizi hayo tu ilhali Israel ilitumia pia mabomu yanayoathiri seli za mwanadamu ambazo ni hatari mno kuliko mabomu ya fosforasi nyeupe.
Amesisitiza kuwa Israel imekiuka sheria zote za kimataifa na kibinadamu na kudhihirisha sura yake ya kinyama kwa walimwengu katika mashambulizi ya siku 22 dhidi ya raia wa Gaza.
Mkutano wa Waendesha Mashtaka wa nchi za Kiislamu na wanasheria wa kimataifa wa Tehran umefanyika kwa lengo la kuchunguza njia za kuwafuatilia kisheria watenda jinai za kivita na mauaji ya kizazi ya raia wa Gaza yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel. 393119