IQNA

Human Rigts Watch yaukosoa utawala haramu wa Israel kwa kuficha jinai za Gaza

8:52 - April 25, 2009
Habari ID: 1769093
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limekosoa vikali hatua ya utawala haramu wa Israel ya kufanya uchunguzi kuhusiana na vitendo vya askari wake katika mauji ya umati huko katika Ukanda wa Gaza na kusema kuwa huko ni kujaribu kuficha jinai zake dhidi ya wakazi wasio na hatia wa Gaza katika hujuma ya kinyama ya siku 22 katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Islamonline, Joe Stork, Naibu Mkuu wa shirika hilo ametoa taarifa akisema kuwa natija za awali zilizotangazwa na utawala wa Israel kuhusiana na suala hilo zinaonyesha wazi kwamba utawala huo unajaribu kufunika ukiukaji wa sheria za kimataifa uliotekelezwa na askari wake dhidi ya watu wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza.
Jenrali Dan Halutz, Naibu Kamanda Mkuu wa Majeshi ya utawala ghasibu wa Israel alitangaza siku ya Jumatano kwamba kwa mujibu wa chunguzi tano tofauti zilizofanyika kuhusiana na suala hilo, matokeo yake yameonyesha kwamba askari wa utawala huo hawakuhusika na vitendo vyovyote vya ukiukaji wa sheria za kimataifa wala uvunjaji wa haki za binadamu katika hujuma hiyo. Amedai kwamba askari hao waliheshimu na kutekeleza kikamilifu sheria za kimataifa pamoja na kuchunga misingi ya maadili na utaalamu wa kijeshi katika hujuma hiyo ya kinyama iliyolaaniwa na ulimwengu mzima!
Huku likipinga vikali matamshi ya watawala wa Israel kuhusiana na suala hilo, shirika la Human Rights Watch limesisitiza kwamba uchunguzi wake na wa taasisi nyinginezo za kimataifa unathibitisha kuwa askari hao walihusika moja kwa moja katika uvunjaji wa haki za binadamu, moja ya mifano ya wazi ikiwa ni kitendo cha askari wa utawala huo kushambulia kwa mabomu makazi ya raia na utumiaji wa silaha zilizopigwa marufuku za fosforasi nyeupe dhidi ya raia. Madaktari wa nchi za Kiarabu na kimataifa walithibitisha mara kadhaa kwamba utawala wa Israel ulitumia silaha hizo zilizopigwa marufuku dhidi ya raia ambao waliathirika sana kutokana na madhara ya silaha hizo.
Mauaji hayo ya kinyama ya siku 22 yaliyotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza tokea tarehe 27 Disemba mwaka uliopita yalipelekea zaidi ya watu 1400 kuuawa wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake. 393655
captcha