Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP, Waziri Zaqzuq amesema kuwa kama wanavyohiji katika mji wa makka kila mwaka, Waislamu wanapasa kufanya safari na kuzuru Quds Tukufu kila mwaka ili kuuweka chini ya mashinikizo utawala haramu wa Israel na kuufanya usimamishe vitendo vyake vya uharibifu katika eneo hilo.
Zaqzuq amesema, kwa kufanya safari kama hizo kila mwaka katika eneo la Masjidul Aqsa, Waislamu wataulazimisha utawala huo wa kidhalimu kukubali kutambua mji wa Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa taifa la Palestina.
Huku akikiri kwamba matamshi yake hayo yataamsha hasira ya watawala wa Israel, Waziri Zaqzuq amesisitiza kwamba Waislamu wanapasa kutekeleza hatua hiyo mara moja hata kama ni kwa kuomba viza ya kuingia katika eneo hilo takatifu, ambalo ni kibla cha kwanza cha Waislamu, kutoka kwa utawala huo haramu.
Waziri wa Wakfu wa Misri amesema kuwa iwapo pendekezo lake hilo litakubaliwa na kutekelezwa na Waislamu wote ni wazi kuwa dunia nzima italazimika kukubali kwamba mji wa Quds Tukufu ni mji mkuu wa taifa la Palestina. 393624