IQNA

Nchi za Kiislamu zina nafasi kubwa katika kudumisha amani ya kimataifa

10:43 - April 25, 2009
Habari ID: 1769268
Waziri wa Sheria wa Senegal amesema kuwa nchi za Kiislamu zina nafasi kubwa katika kudumisha amani ya kimataifa na akasisitiza kwamba kuhitimishwa mgogoro wa Palestina kutakuwa hatua kubwa katika njia ya kufikia lengo hilo.
Madicke Niang ameliambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) kwamba nchi za Kiislamu zinaweza kuwa na mchango muhimu katika kurejesha amani ya kimataifa lakini jambo hilo haliwezekani bila ya kuwepo umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Waziri wa Sheria wa Senegal ambaye ameshiriki katika mkutano wa Waendesha Mashtaka wa nchi za Kiislamu na wanasheria wa Kimataifa mjini Tehran amesema kuwa mjadala wa ubaguzi wa Wazayuni na mauaji ya umati yaliyofanywa dhidi ya wananchi wa Palestina hauhusu ulimwengu wa Kiislamu pekee bali walimwengu wote wanaelewa kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel umetekeleza jinai za aina mbalimbali ili kufikia malengo yake katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina. Niang amesisitiza kwamba walimwengu wanapaswa kushirikiana na kuwafikisha mahakamani viongozi wa utawala ghasibu wa Israel.
Waziri wa Sheria wa Senegal amesifu misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kutatua masuala ya ulimwengu wa Kiislamu na akasema: Iran daima imekuwa mstari wa mbele katika kuitisha mikutano ya kimataifa ya kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu na kudumisha mshikamano na udugu baina ya nchi za Kiislamu.
Madicke Niang amesema kuwa kuwasaidia wananchi wa Gaza ni wajibu wa Waislamu wote na kwamba wakati umefika kwa Waislamu kusimama wima kwa ajili ya kuwatetea watu wa eneo hilo. 393591
captcha