Abduladhim al Maghribi amesema kuwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu zimeanza kufuatilia kisheria suala la kufikishwa mahakamani watenda jinai wa utawala ghasibu wa Israel kupitia mahakama mbalimbali duniani kama huko Hispania, Uingereza na Canada. Amesema kwa sasa jumuiya hizo mbili zinakusanya ushahidi na nyaraka mbalimbali za kuwasilisha katika mahakama za kimataifa kama ile ya The Hague kwa ajili ya kuwafuatilia watenda jinai wakuu sita wa Israel akiwemo Waziri Mkuu wa zamani wa utawala huo Ehud Olmert.
Mwanasheria huyo wa kimataifa wa Misri ambaye ameshiriki katika mkutano wa kimataifa wa Waendesha Mashtaka wa nchi za Kiislamu na wanasheria wa kimataifa amesema kuwa yeye mwenyewe anafuatilia suala la kufanyiwa mabadiliko sheria za Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama na kutekelezwa uadilifu kikamilifu. 393553