Hayo yamesemwa na Imam wa msikiti wa mji wa Kashmar huko kaskazini mwa Iran Hujjatul Islam Sayyid Qasim Yaaqubi. Amesema kuwa maadui wa Uislamu walijaribu kuvuruga mkutano wa Geneva wakati Rais Ahmadinejad alipokuwa akihutumia mkutano huo lakini ushujaa, azma kubwa na moyo wa kimapinduzi wa Rais Ahmadinejad ulimuwezesha kufikisha sauti ya ulimwengu wa Kiislamu kwa walimwengu.
Sheikh Qasim Yaaqubi ameashiria uchaguzi ujao wa rais nchini Iran na akawataka wagombea kuwa na takwa ya kisiasa na kumuoga Mwenyezi Mungu katika kampeni za uchaguzi huo. 393909