Abbas Ali Kadkhudai ameyasema hayo katika kongamano la "Haki za Binadamu, Kuanzia Nadharia hadi Matendo" mjini Tehran na kuongeza kuwa wataalamu na wanasiasa kote duniani wameliweka suala la haki za binadamu katika siasa zao kuu. Amesema kuwa katika miongo miwili ya hivi karibuni wasomi na wanasiasa duniani wamelipa umuhimu mkubwa suala la haki za binadamu kutokana na umuhimu wake.
Kadkhudai amesema kuwa suala hilo limekuwa wenzo wa kisiasa unaotumiwa na madola makubwa kwa ajili ya kuidhibiti dunia.
Msemaji wa Baraza la Kulinda katiba amesisitiza kwamba kuna udharura wa kutambulika vyema haki za binadamu na kujadiliwa katika duru za kielimu. 395516