IQNA

Kuwapenda Ahlul Bait wa Mtume, nguzo ya umoja wa Kiislamu

14:41 - April 28, 2009
Habari ID: 1771159
Waislamu wanapaswa kuwa macho mbele ya njama za kuwatenganisha zinazofanywa na maadui wa dini hiyo na wanapaswa kulifanya suala la kuwapenda Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume (saw) kuwa nguzo ya umoja na mshikamano baina yao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Ulinganiaji wa Kiislamu ya eneo la Mahinshan nchini Iran Sheikh Abbasi ambaye ameongeza kuwa Waislamu wote wanashirikiana katika kuwapenda Watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Muhammad (saw) na kwamba suala hilo linapaswa kuwa nguzo ya umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Amesisitiza juu ya udharura wa kuwatambua Maimam kutoka Nyumba ya Mtume (saw) na kuiga mwenendo wao katika kuimarisha umoja wa Kiislamu.
Sheikh Abbasi amewataka pia Waislamu kuwa macho zaidi katika kukabiliana na njama mbalimbali za maaadui na kusisitiza kuwa suala hilo litasaidia juhudi za kuimarisha umoja baina ya Waislamu. 395397

captcha