Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, maneno hayo yamesemwa na Lina Larsen, mhadhiri wa masuala ya Kiislamu katika mji wa Oslo, ambao ni mji mkuu wa Norway na mwanachama wa zamani wa Baraza la Waislamu wa nchi hiyo. Kwa msingi huo amesisitiza juu ya udharura wa kutolewa mafunzo na malezi ya kutosha kwa wahubiri wa Kiislamu wanaotumwa katika nchi za Magharibi ili waweze kutekeleza vyema majukumu yao kwa mujibu wa mahitaji ya zama na mazingira wanamoishi.
Amesema, kuimarishwa mazungumzo ya pande mbili za Kiislamu na nchi za Magharibi kupitia kubainishwa nafasi ya ustaarabu wa Kiislamu katika maendeleo na ustawi wa jamii ya mwanadamu, msimamo wa Uislamu kuhusiana na ugaidi na maisha ya pamoja ya amani kati ya mataifa na tamaduni mbalimbali ni jambo lenye umuhimu mkubwa.
Akizungumzia baadhi ya huduma zinazotolewa na Baraza la Waislamu wa Norway kwa Waislamu wa nchi hiyo, Lina Larsen amesema kuwa baraza hilo linashughulikia masuala mbalimbali ya Waislamu yakiwemo ya kidini, kisiasa, kiutamaduni na kisheria na kusema kuwa kimsingi baraza hilo ndilo daraja la kuwaunganisha Waislamu na serikali ya nchi hiyo. Akizungumzia vitendo vya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu ambavyo vimekuwa vikienezwa na nchi za Magharibi Larsen amesema kuwa vitendo kama hivyo vinaweza kuondolewa tu kupitia mazungumzo yenye nia njema ya pande mbili na kwa lengo la kuelimishana. 396113