Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Hani Nadhir Aziz anayemiliki weblogu ya "Karzul Hubb" alitiwa nguvuni na askari usalama wa Misri Jumatatu ya wiki hii kwa kosa la kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Mkurugenzi wa Kanali ya Mawasiliano ya Haki za Binadamu ya Kiarabu Jamal Iddi amesema kuwa jumuiya hiyo inafuatilia kadhia ya kutiwa nguvuni mwanaweblugu huyo wa Misri.
Wakili wa Hani Nadhir Aziz amesema kuwa askari usalama wa Misri wamekataa kuamuachia huru kwa dhamana kwa hoja kwamba maisha yake huweka yakawa hatarini.
Aziz amekuwa akifanya kazi kama mtaalamu wa masuala ya kijamii katika shule moja ya mkoa wa Qana nchini Misri. 396031