Barala Kuu la Kitaifa la Tamasha la Quds, Mji Mkuu wa Ulimwengu wa Kirabu mwaka 2009, limelaani hatua ya utawala haramu wa Israel ya kujenga hekalu chini ya shule ya kihistoria ya al-Tankazia karibu na Msikiti wa al-Aqsa.
Katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo kupitia shirika la habari la Wafa, baraza hilo limesema kuwa hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni ni hujuma ya wazi dhidi ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kiarabu na kwamba inakiuka pia misingi na sheria za kimataifa.
Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa hekalu hilo litakuwa ndilo hekalu kubwa zaidi ulimwenguni na kwamba limepangiwa bajeti ya ujenzi ya dola milioni arubaini.
Ili kutekeleza mradi huo, utawala wa Kizayuni umepanga kubomoa nyumba za Wapalestina zipatazo 50 katika eneo la al-Bustan la Baitul Muqaddas. 397714