IQNA

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki akosoa marufuku ya hijabu nchini humo

10:23 - May 02, 2009
Habari ID: 1772387
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki amekosoa vikali siasa za nchi hiyo za kupiga marufuku vazi la stara kwa mwanamke wa Kiislamu, hijabu katika vituo vya elimu ya juu na hasa katika vyuo vikuu na kusema kuwa jambo hilo linakinzana wazi na haki za kimsingi za binadamu na uhuru wake.
Shirika la habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRNA limeripoti kuwa, Nimet Cubukcu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ambaye alikuwa akizungumza pambizoni mwa kikao cha Kamisheni ya Haki za Wanawake na Usawa wa Jinsia ya Ulaya amesema kuwa, wanawake wengi wa Kiislamu wanalazimika kuvaa hijabu kutokana na mafundisho ya dini yao tukufu. Amemaliza kwa kusema, iwapo baadhi ya watu watanyimwa huduma kutokana na fikra zao za kidini kwa hakika watakuwa wamenyimwa haki zao za kimsingi za kibinadamu.
Amesema kuwa utamaduni wa kihafidhina usiotambua rasmi thamani za wanawake na kuwazuia kuhudumu katika shughuli za juu katika mashirika na taasisi mbalimbali unazidi kupata nguvu katika baadhi ya nchi na jamii.
Ameelezea masikitiko yake makubwa kwamba kwa bahati mbaya fikra hizo potofu zinaenezwa na baadhi ya makundi ya Kiislamu kwa jila la dini tukufu ya Kiislamu. Amesema hii ni katika hali ambayo Uislamu unapinga vikali upotofu huo na kusema kuwa mwanamke na mwanaume wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. 397701
captcha