Kwa mujibu wa tovuti hiyo, mpango huo ulianza mwaka mmoja uliopita sambamba na kumbukumbu ya shahada ya Shahid Murtadha Muttari, mwanafikra wa Kiislamu, kwa lengo la kueneza utamaduni wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo wasomaji husajili majina yao kupitia mtandao kwa lengo la kusoma na kukamilisha juzuu moja ya Qur'ani ambapo kila siku juzuu zote za 30 za Qur'ani husomwa na wasomaji kunufaika na thawabu za shughuli hiyo.
Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwa uchache siku moja katika kila mwezi imetengewa usomaji Qur'ani huo na shughuli hiyo kufanyika kila siku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Nukta ya kuvutia hapa ni kwamba, baadhi ya wakati jamaa wa familia nzima hushiriki katika jambo hilo la kheri.
Kwa kukaribia kutimia mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa tovuti hiyo, watu walio na hamu ya kushiriki katika shughuli hiyo wameombwa kusajili majina yao na kuchagua juzuu wanazopendelea kusoma kupitia anwani ifuatayo: www.iec-md.org.
Ratiba ya msimu huu wa kuchipua ni pamoja na kukamilisha usomaji Qur'ani mara mbili katika siku za Jumamosi Mei Pili ambayo inasadifiana na siku ya kuuawa shahidi Ustadh Muratadha Mutahhari na Alkhamisi Mei 7 sambamba na kuwadia siku ya kuuawa shahidi Bibi Fatma Zahra (as) binti ya Mtume Muhammad (saw). 397671