IQNA

Kitabu cha ‘Sifa Kuu za Madrasa Mbili’ chafasiriwa kwa Kiswahili

8:31 - May 04, 2009
Habari ID: 1773469
Kitabu kiitwacho ‘Sifa Kuu za Madrasa Mbili’ (Ma'alimul Madrasatain) kilichoandikwa na Ayatullah Sayyid Murtadha Askari kimefasiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kitabu cha ‘Sifa Kuu za Madrasa Mbili’ kimetarjumiwa kwa ushirikiano wa Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania na Taasisi ya Uchapishaji na Ufasiri ya Al Itrah. Kitabu hicho kimefasiriwa kutoka lugha ya Kifarsi.
Kitabu hicho kinajadili masuala ya misingi ya itikadi za madhehebu za Kiislamu za Suni na Shia na kulinganisha itikadi hizo mbili. Aidha kitabu hicho chenye juzuu tatu kinachunguza na kujadili masuala ya vyanzo vya sheria za Kiislamu, Suna za Mtume (SAW), harakati wa Imam Hussein (AS) na kadhalika.
Vitabu vingine vilivyoandikwa na mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu ni pamoja na Abdullah bin Saba, Itikadi za Uislamu Katika Quran Tukufu, Nafasi ya Maimamu Katika Kuhuisha Dini n.k
398578
captcha