IQNA

Juhudi za kuimarisha misingi ya kiroho katika Jamii

17:26 - May 05, 2009
Habari ID: 1774067
Ayatullah Nuri Hamedani ametoa wito kwa maafisa wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuzidisha masuala ya kiroho na kimaanawi katika jamii.
Akizungumza na Mkurugenzi na maafisa wa Shirika la Ulinzi wa Kiraia, mwanazuoni huyo mwadamizi amesema kuwa mpango wa kuimarisha misingi ya kiroho katika jamii ni jambo linalotiliwa mkazo pia na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Amesema suala hilo pia ni wadhifa wa Waislamu wote na kuongeza kuwa kila mwanadamu mwenye akili ni lazima azitambua ipasavyo zama aishizo.
Ayatullah Hamedani amesema, moja kati ya sifa za kipekee za Imam Khomeini (SA) ni kutambua zama. Amesema jambo hili lilimuwezesha kufanikiwa na kuweza kuarifisha harakati ya wananchi kwa walimwengu na hatimaye kuifanikisha harakati hiyo. Mwanazuoni huyo ameongeza kuwa, lengo la mapinduzi ni kuarifisha dini na kuwarejesha watu katika Uislamu halisi na kwamba watu wote wanapaswa kushirikiana katika kufikia lengo hili.
Ayatullah Hamedani amesisitiza kuwa, 'kutambua zama humpa mwanadamu istiqama na kwamba ustawi unahitajia subira na ukakamavu'. 399168
captcha