IQNA

Umoja kati ya madhehebu ni haja ya siku nyingi ya umma wa Kiislamu

17:22 - May 05, 2009
Habari ID: 1774116
Hujjatul Islam Jawadi Amoli amesema kuwa umoja na mshikamano kati ya wafuasi wa madhehebu mbalimbali za Kiislamu ni haja ya siku nyingi ya umma wa Kiislamu ambayo daima imekuwa ikisisitizwa na wanafikra na wanamageuzi wa kidini.
Hujjatul Islam Jawadi Amoli ameyasema hayo katika kongamano la Umoja wa Kiislamu na Shahid Mutahhari mjini Doha Qatar. Sheikh Amoli ametoa wito wa kustawishwa ustaarabu wa Kiislamu, kueneza adabu na maadili mema, ustawi na hali bora ya kimaada kwa ajili ya mataifa yote na kuimarishwa zaidi misingi ya uvumilivu wa kidini kwa kutumia vigezo vya mafundisho ya Qur'ani.
Amesema kuwa elimu ni nuru inayomfunulia mwanadamu asiyoyajua na kwamba wanazuoni wa kidini wanawaondoa wanadamu katika giza la ujinga na kuwaelekeza kwenye mwanga na ubinadamu.
Amesema kuwa shahid Murtadha Mutahhari alishughulikia mno suala la umoja kati ya Waislamu na kadhia ya Palestina.
Kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na wasomi na wanafikra mbalimbali wa Kiislamu limehutubiwa pia na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Qatar na shakhsia wengine kadhaa. 399365




captcha