IQNA

Hamas: Nchi za Kiarabu ndizo zinazopazwa kulaumiwa kwa mzingiro wa Gaza

11:45 - May 06, 2009
Habari ID: 1774767
Harakati ya Hamas imesema kuwa viongozi wa nchi za Kiarabu ndio wanaopaswa kulaumiwa kutokana na kuendelea mzingiro wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza.
Hamas imewataka viongozi wa nchi za Kiislamu kuchukua hatua mpya za kukabiliana na hatua zisizokuwa za kisheria za utawala ghasibu wa Israel.
Msemaji wa Hamas Fauzi Barhum amesema kuwa idadi kadhaa ya wananchi wa Palestina wanafariki dunia kila siku kutokana na mzingiro huo huku viongozi wa nchi za Kiarabu wakinyamaza kimya na kushuhudia kwa macho tu mashaka ya Wapalestina.
Amesema msimamo wa viongozi wa Kiarabu kuhusu mauaji makubwa ya Israel huko Gaza ulikuwa dhaifu mno na akaongeza kuwa inashangaza kuona bendera ya utawala ghasibu wa Israel ikipepea katika baadhi ya nchi za Kiarabu huku raia wa Palestina wakiendelea kuteseka kwa mzingiro wa pande zote wa Wazayuni.
Amesema kuwa inashangaza kuona kwamba vikao vya nchi za Kiarabu vilivyofanyika katika nchi za Qatar, Misri, Kuwait na Saudi Arabia vimeshindwa kuvunja mzingiro wa Israel dhidi ya eneo la Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa Hamas amezihimiza tena nchi za Kiarabu na Kiislamu kufanya juhudi zaidi za kukomesha mzingiro huo ambao unaendelea kuwatesa raia wa Gaza tangu mwaka 2007. 400136

captcha