IQNA

Kuanza mkutano wa kimataifa wa "Sira ya Mtume katika Mtazamo wa Wasomi wa Marekani."

11:46 - May 06, 2009
Habari ID: 1774773
Mkutano wa kimataifa wa kuchunguza sira ya Mtume katika athari na maandiko ya wataalamu wa masuala ya mashariki wa Marekani ulianza jana Jumanne katika mji wa Fas nchini Morocco.
Mkutano huo unaosimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Morocco unahudhuriwa na wasomi, watafiti na wahakiki kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu na Marekani.
Ajenda kuu ya mkutano huo ni kuchunguza historia ya utafiti na maandiko ya wataalamu wa masuala ya Mashariki (orientalist) wa Marekani kuhusu sira ya Mtume Muhammad (saw) na mbinu zao katika utafiti huo.
Maudhui nyingine zinazojadiliwa ni taswira ya Mtume Mtukufu katika mijadala ya kidini, fasihi, mbinu mbalimbali za masomo, vyombo vya habari na tafiti za wasomi na wataalamu wa Marekani wa masuala ya nchi za Mashariki. 399962

captcha