Katika mkutano wao wa mwaka Mei 5, wabunge hao wa Lebanon wametoa taarifa na kulaani hatua za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel za kuharibu nyumba za Wapalestina pamoja na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni mjini Baitul Muqaddas. Wamesema lengo la Wazayuni ni kuupa sura ya Kiyahudi mji wa Baitul Muqaddas. Wameutaka Umoja wa Mataifa utekeleze majukumu yake na kuushurutisha utawala wa Kizayuni kusitisha sera zake za Kuuyahudisha mji wa Baitul Muqaddas.
Washiriki katika kikao hicho walisisitiza kuwa utawala wa Misri unapaswa kuacha kushirikiana na utawala wa Kizayuni na kuondoa mzingiro dhidi ya eneo la Wapalestina la Ukanda wa Ghaza. Wabunge hao wa Lebanon katika taarifa yao aidha wamesema kuna haja ya kutekelezwa kivitendo mapatano ya makundi ya Kipalestina ya kuleta umoja baina yao.
Aidha wamesema kuwa makundi ya wanamapambano yana nafasi muhimu katika kifichua njama za Wazayuni na kuonya kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel unapanga njama za kuzua mifarakano miongoni mwa Walebanon.
400596