Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Lebanon, Allamah Fadlallah amesema, ‘Tokea ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hadi sasa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikihujumiwa na maadui kwa visingizio mbali mbali lakini nchini hii ingali dola lenye nguvu na inasimama kidete na kutumia uwezo wake wote katika kukabiliana na maadui wa Ummah wa Kiislamu’.
Ameyasema hayo mjini Beirut katika mkutano wake na Manuchehr Mohammadi, mshauri wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pamoja na wataalamu kadhaa wa Taasisi ya Imam Khomeini (SA) yenye makao yake katika mji wa Qum nchini Iran.
Allamah Fadlallah amezungmzia jitihada zenye thamani za Imam Khomeini (SA) katika kuibadilisha Iran kuwa dola lenye nguvu kwa manufaa ya Waislamu na kusema: ‘Imam (SA) aliifanya Iran kuwa nchi huru na ifuatayo uadilifu na isiyo salimu amri mbele ya mashinikizo ya kimataifa’.
Ameongeza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa ni nchi ambayo inatetea mataifa yanayodhulumiwa duniani na taifa la Palestina liko katika kilele cha mataifa yanayopewa himaya na Iran.
Marajaa huyo wa Mashia wa Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni hitajio muhimu la Waarabu na Waislamu. Ametoa wito kwa viongozi wa Iran kudumisha umoja walionao na pia kufanya juhudi za kuwanunganisha Waisalmu wote duniani. 401589