IQNA

Matamshi mazuri ya balozi wa Uholanzi nchini Indonesia yamkasirisha mbunge mwenye misimmo ya chuki dhidi ya Uislamu

12:26 - May 09, 2009
Habari ID: 1775780
Mbunge mwenye misimamo ya kupindukia na chuki dhidi ya Uislamu wa nchini Uholanzi amekosoa vikali matamshi mazuri yaliyotolewa hivi karibuni na balozi wa nchi hiyo kuhusu Uislamu.
Kwa mujibu wa gazeti la Indonesia Jakarta Post, Geert Wilders, mbunge wa Uholanzi mwenye chuki dhidi ya Uislamu amesema kuwa, matamshi ya Balozi Nicholas Vandam kwamba Uislamu umekuwa na mchango mzuri katika mwenendo wa siasa za ulimwengu ni jambo lisilokubalika kabisa. Balozi huyo alitoa matamshi hayo alipokuwa akihutubu hivi karibuni katika Taasisi ya Utafiti wa Qur'ani mjini Jakarta kuhusiana na nafasi ya Uislamu na wanafikra wa Kiislamu katika mwenendo wa siasa za dunia. Katika taarifa aliyotoa kupitia mtandao wake wa www.islamiswar.org mbunge huyo anayeendesha vita dhidi ya Uislamu na Waislamu amedai kwamba kwa matamshi yake hayo, Balozi Vandam badala ya kuwa mwakilishi wa taifa na serikali ya Uholanzi nchini Indonesia amejifanya kuwa mfuasi na muungaji mkono wa Uislamu na hivyo kujipotezea itibari. Mbunge huyo ambaye ametengeneza filamu ya matusi na dharau dhidi ya Uislamu iitwayo Fitna amesema kwamba badala ya balozi huyo kuutetea Uislamu alipaswa kutetea haki za binadamu na kujaribu kuimarisha nafasi ya Wakristo waliowachache nchini Indonesia. Pia amemkosoa vikali balozi Vandam kwa kusema kuwa nchi ya Kiislamu ya Uturuki ni nchi ya Ulaya. Wilders na wanachama wenzake wamemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi wakimtaka amfukuze kazi balozi Vandam. 401614
captcha