Afisa mwandamizi wa Banki Kuu ya Singapore amesema Noti za Kiislamu za dhamana (Islamic bonds )maarufu kama Sukuk* zitachapishwa Singapore, Malaysia, na Indonesia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA kusini-mashariki mwa Asia, afisa huyo kifedha wa Singapore amongeza kuwa, noti hizo mpya za Kiislamu kwa ujumla zitakuwa na thamani ya dola bilioni 1.3 na zitachapishwa katika nusu ya pili ya mwaka 2009.
Heng Swee Keat Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Singapore amesema noti za Kiislamu za dhamana za serikali zitachapishwa awali kwa ajili ya Benki ya Kiislamu ya Asia na kwamba atachunguza maombi ya benki zinginezo zinazotaka kunufaika na noti hizo'.
Amesema inatabiriwa kuwa inatarajjiwa kuwa watakaomiliki noti hizo za dhamana katika sekta ya binafasi watanufaika na soko la sukuk na hivyo kuwavutia wawekezaji wapya.
Itakumbukwa kuwa mapema mwaka huu mwezi wa Januari ilianzisha mkakati wa kuchapisha Noti za Kiislamu za dhamana na kufanikiwa kuchapisha noti zenye thamani ya dola milioni 200 ambazo zilitumika katika biashara na Malaysia kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
*Sukuk ni mfumo wa kudhamini fedha kwa mujibu wa sheria za Kiislamu pasina kuwepo riba na hutumika kama cheti cha uwekezaji. 401675