IQNA

Qur'ani iliyoandikwa kwa mkono yenye umri wa miaka 800 nchini Uchina

12:26 - May 11, 2009
Habari ID: 1776755
Kuna Qur'ani ya kale iliyo na umri wa miaka 800 na iliyoandikwa kwa mkono inayohifadhiwa katika kijiji cha Qinghai katika jimbo linalojitawala lenyewe la Qinghai kaskazini magharibi mwa Uchina.
Kabila la Salar ni moja ya makabila ya Waislamu waliowachache nchini Uchina ambalo linaishikatika kijiji cha Qinghai, ambacho kina wakazi wapatao laki moja. Qur'ani hiyo inahifadhiwa katika msikiti wa Ghaizi. Qur'ani hiyo inasemekana kuwa moja ya nuskha saba zilizoandikwa kwa mkono katika zama za utawala wa Othman bin Affan, khalifa wa tatu na kabla ya kuwekwa irabu katika maandishi ya Qur'ani. Kwa kuzingatia kuwa Qur'ani hiyo imekuwa ikitumiwa sana na hivyo karatasi zake kuchakaa na kuwa kuukuu, serikali ya Uchina iliamuru wataalamu kadhaa wa mambo ya kale kuikarabati Qur'ani hiyo, shughuli ambayo ilichukua muda wa mwezi mmoja. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji hichohicho cha Qinghai. Kwa muda wa miaka 30, Waislamu wa kijiji hicho walifanya juhudi za kuitoa nuskha hiyo ya Qur'ani kutoka katika jumba la mambo ya kale na kihistoria la mjini Peking, na kwa msingi huo hawakuridhishwa na juhudi za kutaka kukitoa kitabu hicho katika kijiji hicho kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. 402400
captcha