Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa OIC, Ihsanoglu amesema, ‘mapigano na umwagaji damu katika Misikiti ya Somalia na kuvunjiwa heshima makaburi nchini humo ni jambo linalopelekea Wasomali wasio na hatia kupoteza maisha yao’.Amelaani yanayojiri Mogadishu hivi sasa na kusema hayakubaliki.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu amewataka wanaozusha vita kusitisha uhasama wao mara moja ili kuzuia nchi hiyo ya pembe ya Afrika kutumbukia katika maafa mengine.
Aidha ameyataka makundi yote ya upinzani Somalia kuafikiana na serikali mpya ya mpito ili amani ya kudumu ipatikane nchini humo.
Ihsanoglu aidha amesema Jumuiya ya Nchi za Kiislamu itashirikiana na jamii ya kimataifa ili kuyasaidia makundi ya Somalia kurejesha amani ya kudumu katika nchi hiyo. 403973