Kwa mujibu wa gazeti la ar-Rayya, Ali bin Abdallah as-Suweidi mkuu wa taasisi hiyo amesema kuhusiana na suala hilo kwamba tayari taasisi hiyo imetenga kiasi cha dola laki moja kwa madhumuni ya kuwasafirisha Wapalestina wanaoishi katika maeneo mengine ya ardhi zinazokoliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel na kuwapelaka katika Msikiti wa al-Aqsa ili kuswali katika eneo hilo takatifu. Amesema, uungaji mkono kwa athari za Kiislamu na kihistoria za msikiti wa al-Aqsa, mipango ya elimu, kisheria na kihubiri kwa wakazi wa Quds ni miongoni mwa mipango mingine iliyopangwa kutekelezwa na taasisi hiyo ya Id bin Muhammad Aali Thani, kwa ushirikiano wa Taasisi ya Kimataifa ya Quds. As-Suweidi ameendelea kusema kuwa, moja ya mipango ya mafunzo na uhubiri ambayo imepangwa kutekelezwa na taasisi iliyotajwa ya Qatar huko Quds, ni kutengwa dola milioni moja kwa madhumuni ya kujenga vituo vya elimu na shule ya mabinti wa wakimbizi wa Kipalestina na pia kutengwa dola laki 6.65 kwa shabaha ya kujengwa kituo cha shughuli za uhubiri na utamaduni wa Kiislamu. As-Suweidi amesema mwishoni kwamba, Quds na Msikiti wa al-Aqsa vimekita mizizi katika nyoyo za Waislamu kote ulimwenguni na kwamba kutekelezwa kwa mipango hiyo ya kheri ni aina moja ya kudhihirisha upinzani dhidi ya juhudi zinazofanywa kila uchao na maghasibu wa Kizayuni kwa ajili ya kufuta utambulisho halisi wa Quds na kuubadili na wa Kiayahudi. 403972