Kwa mara ya kwanza kabisa, mfumo wa kujibu maswali ya kisheria na kidini ya Waislamu kupitia simu, utazinduliwa hivi karibuni nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharqul Ausat, Shirika la Unite la Uingereza ambalo limepewa tenda ya kushughulikia suala hilo limesema kuwa, tokea sasa Waislamu wa Uingereza wataweza kujua fatuwa za wanazuoni mashuri wa ulimwengu wa Kiislamu wakiwemo wa al-Azhar kuhusiana na masuala mbalimbali na pia kuuliza na kujibiwa maswali yao kuhusiana na masuala tofauti ya kidini kutoka kwa wanazuoni pamoja na wasomi wa Kiislamu. Katika taarifa iliyotolewa na shirika hilo, maswali na majibu yatakayotolewa kupitia mfumo huo yatatimia katika lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kiurdu, na kwamba gharama ya kila dakika ya mazungumzo kupitia mfumo huo ni karibu dola moja. Mfumo huo umepangwa kuzinduliwa mwezi ujao na utakuwa ukifanya kazi kwa muda wa masaa 24 kila siku ambapo Waislamu wa Uingereza watapata nafasi ya kuuliza na kujibiwa maswali yao kuhusiana na masuala yao mbalimbali ya kidini na kimaisha. Hivi sasa mifumo kama hiyo inatumika katika nchi kadhaa za Kiarabu zikiwemo za Misri, Imarati, Syria, na Paletina. Uingereza ni nchi ya kwanza isiyo ya Kiislamu kuzindua mfumo huo wa simu wa maswali na majibu ya kidini kwa Waislamu. 403937