IQNA

Mashia wa Uingereza waandamana mbele ubalozi wa Saudia nchini Uingereza

17:01 - May 16, 2009
Habari ID: 1779040
Mashia wa Uingereza siku ya Ijumaa alasiri walifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia wakilalamikia fatua zilizotolewa hivi karibuni na mamufti wa Kiwahabi wa Saudi Arabia katika kuwakufurisha Mashia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la As'watul Iraq, mara tu baada ya kutoa fatuwa ya kukufurisha na kuhalalisha damu ya Mashia katika mahojiano yake ya hivi karibuni na televisheni ya BBC ya nchini Uingereza, Adel Kalbani, Mufti wa kiwahabi wa Saudi Arabia ambaye pia ni Imam wa Jamaa wa Msikiti Mtakatifu wa Makka alikabiliwa na malalamiko makubwa ya Mashia kote ulimwenguni. Maandamano ya Mashia wa Uingereza ni sehemu moja tu ya maandamano hayo ambayo yamekuwa yakifanywa na Mashia kulalamikia fatuwa hiyo. Taarifa iliyotolewa na Mashia hao inamtaka mfalme wa Saudi Arabia kumuuzulu mara moja mufti huyo na kuweka mahala pake imam mwingine ambaye atahubiri amani na umoja miongoni mwa Waislamu. Katika mahojiano yake na shirika la BBC ambayo yalifanyika wiki iliyopita, Kalbani aliwakufurisha wanazuoni wa Kishia na kuwachochea mawahabi wenye misimamo ya kupindukia mipaka kumwaga damu na kuwaua wafuasi wa madhehbu hii muhimu ya Kiislamu. 405404
captcha