IQNA

10:20 - May 17, 2009
Habari ID: 1779260

Maulamaa wa Kishia na Kisunni watakiwa kushirikiana

Matatizo ya Ulimwengu wa Kiislamu hayawezi kutatuliwa kupitia kuyavunjia heshima matukufu ya Kishia au Kisunni bali njia pekee ni kupitia ushirikiano wa kimaoni wa Maulamaa wa Kishia na Kusunni.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika mkoa wa Sistan na Baluchistan nchini Iran , hayo yamesemwa na Molavi Abdul Hamid Ismail Imam wa Msikiti wa Masunni mjini Zahedan. Ametoa shukrani zake kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Sayyed Ali Khamenei ambaye katika safari yake mkoani Kurdistan alisema, Shia au Sunni anayeyavunjia heshima matukufu ya mwingine ni kibaraka wa maadui. Ametoa wito kwa Maulamaa wa Kisunni na Kishia kuzingatia nasaha za Kiongozi Muadhamu.
Molavi Ismail amesema Waislamu hawapaswi kufanya vitendo vya kuwafurahisha maadui bali wanatakiwa kujiepusha na hatua zozote za kuzusha mifarakano na kuvunjiana heshima.
Imam wa Msikiti wa Masunni huko Zahedan amesema yeye binafsi hatamruhusu msomo yeyote wa Kisunni kuwavunjia heshima Mashia. Aidha ametoa wito kwa Maulamaa wote wa Kisunni na Kishia kuwa waangalifu wasitumbukie katika mtego wa maadui wanaopanga njama za kuzusha mifarakano katika safu za Waislamu. 405735
captcha