Wananchi wa Lebanon wamefanya hafla kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuasisiwa utawala haramu wa Israel miaka 61 iliyopita katika ardhi zlizoghusubiwa za Palestina, siku ambayo ni maarufu kwa jina la Nakba au maafa makuu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Beirut, hafla hiyo ya Ijumaa iliandaliwa na Baraza la Kiislamu la Palestina nchini Lebanon na nara yake kuu ilikuwa ni, ‘Quds ni Mji Wetu Mkuu, Siri ni Umoja Wetu’. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wanaharakati, wabunge na viongozi wa Lebanon pamoja na wanaharakati kutoka Palestina.
Mohammad al Ba’albaki Mkuu wa Jumuiya ya Waandishi Habari Lebanon amehutubia hafla hiyo na kusema, ‘Ni mwaka wa 61 tokea Palestina ilipokaliwa kwa mabavu na ardhi hiyo ingali inakaliwa kwa mabavu na adui Mazayuni ambaye anazidisha hujuma yake dhidi ya taifa madhlumu la Palestina kila uchao’. Ameendelea kwa kuashiria uungaji mkono wa Lebanon kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina na kusema Walebanoni wataendelea kupambana bega kwa bega na Wapalestina hadi wazidhibiti tena ardhi zao hasa Quds Tukufu.
Abbas Zaki Balozi wa Iran nchini Lebanon amehutubia hafla hiyo na kusema, ‘miaka 61 imepita tangu Palestina ikaliwe kwa mabavu na Wazayuni lakini taifa la Palestina lingali na nguvu na irada na kwa hivyo mapambano dhidi ya madhalimu yataendelea’. 405653