Kwa mujibu wa Afriqu.net, warsha hiyo iliandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu ISESCO kwa ushirikiano wa Kamisheni ya Kitaifa ya Masomo, Utamaduni na Sayansi ya Libya pamoja na Baraza la Kitaifa la Vijana la nchi hiyo. Wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu kutoka nchi hiyo, Qatar, Tunisia, Algeria, Palestina, Morocco, Misri na Imarati walishiriki katika warsha hiyo muhimu ambapo wamechunguza na kujadili nafasi ya vijana na ushirikishwaji wao katika miradi mbalimbali ya ustawi wa Kiislamu na hasa kuhusiana na masuala ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Waandaaji wa warasha hiyo wamesema kuwa lengo lake kuu ni kutambua nafasi ya tabaka la vijana katika kudhibiti changamoto za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kunyanyua uwezo wao wa kukabiliana na changamoto hizo. 405761