IQNA

Taarifa ya mamarja' wa Najaf kwa mnasaba wa kuaga dunia Ayatullah Bahjat

15:47 - May 20, 2009
Habari ID: 1781010
Maayatullahil Udhma Sayyid Ali Sistani, Bashir Najafi, Is'haq Fayadh na Sayyid Muhammad Said Hakim siku ya Jumatatu walitoa taarifa tofauti wakituma salamu zao za rambirambi na maombolezo kwa mnasaba wa kuaga dunia Ayatullahil Udhma Muhammad Taqi Bahjat.
Katika taarifa hizo, mamarja' hao walimtaja Ayatullahil Udhma Bahjat kuwa nembo halisi ya takwa, irfani na fikra safi ya Kiislamu na kusema kuwa kifo chake kimeacha mwanya mkubwa katika ulimwengu wa Kiiskamu na hasa wa wafuasi wa Watu ya Nyumba ya Mtume (saw). Kwa mnasaba wa kuaga dunia alim huyo mkubwa hauza ya kielimu ya Najaf ilifunwa na misikiti pamoja na vituo vya kidini vya mji huo kubadilika na kuwa maeneo ya maombolezo ya mwanazuoni huyo mashuhuri. 407702
captcha