Mashia hao vilevile wameitaka serikali kumfuta kazi imam huyo na kumuhukumu mahakamani kutokana na hatua yake hiyo ya kigaidi. Waliotia sani taarifa hiyo wameelezea masikitiko na mshangao wao mkubwa kutokana na kimya mbacho kimeonyeshwa na serikali ya Riyadh kuhusiana na fatuwa hiyo ya kichochezi na ya kuwagawanya Waislamu iliyotolewa na Kalbani. Wamesema kuwa kimya hicho bila shaka kinaandaa uwanja wa kutekelezwa ugaidi na kuwapa mamufti wa kiwahabi wa nchi hiyo fursa ya kutoa fatuwa nyingine za kuwakufurisha Mashia. Mashia wa Saudi Arabia wameendelea kusema kuwa kwa mara nyingine tena Kalbani amebainisha fikra zake potofu katika mahojiano yake na televisheni ya BBC, jambo ambalo linaandaa uwanja wa kutokea na kukaririwa ghasia na mivutano ya kimadhehebu na kwamba, matamshi hayo ya kigaidi yanahatarisha umoja wa Waislamu na jamii ya Saudi Arabia. Taarifa hiyo imesisitiza kwamba Baraza la Maulama wa Saudi Arabia halipasi kutoa mwanya wa mufti yoyote yule kujitolea ovyo fatuwa ya kuwakufurisha Waislamu wenzake na hivyo kuandaa uwanja wa kuchochea fitina na mgawanyiko miongini mwa Waislamu wa Saudia. 408306