IQNA

Kikao cha dharura cha Mawaziri wa Afya wa Mashariki ya Kati kujadili usalama wa mahujaji

19:09 - July 18, 2009
Habari ID: 1803521
Mawaziri wa Afya wa nchi za Mashariki ya Kati wanatarajiwa kukutana kwa lengo la kujadili usalama wa kiafya wa mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika ibada ya mwaka huu ya hija.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumatano ijayo mjini Cairo Misri kujadili ugonjwa na homa ya mafua ya nguruwe nchini Saudi Arabia.
Mawaziri hao wanajadili njia za kuzuia maambukizi ya homa ya mafua ya nguruwe kwa mahujaji, kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo duniani hususan katika eneo la Mashariki ya Kati na njia za kukabiliana na maambukizi yake.
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa Saudi Arabia imeahidi kwamba itachukua hatua za dharura za kuzuia maambikizi ya homa ya mafua ya nguruwe miongoni mwa mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kusisitiza kwamba mahujaji hao wanapaswa kupata chanjo ya ugonjwa huo wiki mbili kabla ya kuelekea Makka kwa ajili ya ibada hiyo. :435594



captcha