IQNA

Mnara mkubwa zaidi wa saa kuzinduliwa mjini Makka

19:33 - August 05, 2010
Habari ID: 1967690
Mnara mkubwa zaidi wa saa kote duniani umetengeneza katika mji mtakatifu wa Makka na unatazamiwa kuanza kazi kwa majaribio katika wiki ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mnara huo wa saa umeinuka juu kiasi cha mita 601 na unahesabiwa kuwa mnara mrefu zaidi wa saa kote duniani. Unaweza kuonekana kutokea umbali wa kilomita saba.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa mnara huo ambao ni mrefu kuliko yote duniani wa saa unaelekea upande wa Masjidul Haram na umetengenezwa na wahandisi wa Kijerumani na Kiswisi wakishirikiana na wataalamu kutoka nchi nyingine za Ulaya.
Mnara ambao saa hiyo itawekwa umejengwa kwa kuzingatia usanifu majengo wa Kiislamu na kurasa za saa yake zinaonekana kutokea pande nne. Kurasa hizo za saa pia zitakuwa na jina la Mwenyezi Mungu la "Allah" na mnara huo utakuwa na chombo cha kupandisha juu na kuwarejesha chini watalii. 626662

captcha