Marivan Naqshbandi ameongeza kuwa nakala hizo za Qur'ani ziliingizwa katika eneo la Kurdistan la kaskazini mwa Iraq kutokea Syria na kwamba sasa zimekusanywa kutoka katika maktaba na maduka ya kuuzia vitabu.
Mtandao wa intaneti wa Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini ya serikali ya Kurdistan ya Iraq umeongeza kuwa aya 100 za sura za Yusuf, Raad na Ibrahim zimeondolewa katika nakana hizo za kitabu kitukufu cha Qur'ani ambazo zimechapishwa katika taasisi ya Darul Mahabba nchini Syria.
Naqshbandi amesema kuwa wizara hiyo imeitumia barua taasisi ya Darul Mahabba ikitaka kuchunguzwa kwa kina suala hilo na kutosambaza tena nakala zenye upungufu za Qur'ani Tukufu. Vilevile amewataka wananchi wa Iraq kutotegemea nakala hizo zenye upunguvu. 626876