Uongozi huo umesema kazi za kukarabati maeneo hayo matakatifu ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kuweka viyoyozi vipya kwa ajili ya kuboresha hali kwa watu wataokazuru maeneo hayo matakatifu katika mwezi wa Ramadhani imekwishaanza.
Vilevile kumewekwa taratibu mpya za usafiri ili kusahilisha mambo kwa mahujaji na watu wanaozuru maeneo matukufu ya Makka na Madina katika mwezi wa Ramadhani.
Mwezi mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza katikati ya wiki ijayo katika maeno mengi duniani. 627837