Gazeti la al Intiqad linalochapishwa nchini Lebanon limekinukuu chombo kilicho karibu na Ayatullah Sistani kwamba kiongozi huyo wa ngazi za juu wa kidini wa Iraq hajapokea barua yoyote kutoka kwa Rais wa Marekani na wala hana mawasiliano ya aina yoyote ile na Barack Obama, jeshi la Marekani na ubalozi wa nchi hiyo nchini Iraq.
Chombo hicho kimesisitiza kuwa hata kama Ayatullah Sistani ataingilia kati suala hilo itakuwa si kwa sababu ya matakwa ya Rais wa Marekani bali kwa kuchelea mustakbali wa Iraq.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa hivi karibuni vyombo vya habari vilitangaza habari inayosema kuwa Rais Barack Obama wa Marekani amemtaka kiongozi mkuu wa kidini wa Iraq Ayatullah Sistani kuingilia kati suala la kuundwa serikali mpya ya nchi hiyo. 628848