Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limefanyika kwa mnasaba wa mwaka wa mwaka 2010 ambao umetangazwa kuwa Mwaka wa Quran Tukufu nchini Uturuki. Kati ya waliodhudhuria ni pamoja na Halil Çiçek mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ankara, Sheikh Faruk Arvas Mufti wa mkoa wa Siirt, Sheikh Suat Göztok Imamu na Khatibu wa Msikiti wa Bayzid mjini Istanbul, Musa Çolak Mkuu wa Mkoa wa Siirt, Seyfettin Aydın Naibu Meya wa Siirt pamoja na Maualmaa na wananchi wa Siirt. Baada ya kikao kufunguliwa kwa kusomwa Quran Tukufu, Halil Çiçek alitoa hotuba na kusema walimwengu wameghafilika na madundishi ya kimaanawi ya Quran Tukufu. Ameongeza kuwa: "Iwapo wanaadamu hasa wafuasi wa dini ya Kiislamu watatekeleza mafundisho ya Quran Tukufu, basi matatizo yote ya mwanaadamu yatatatuliwa".
629790