Abdul Jalil al-Makrani, Mkuu wa Kituo cha Qur'ani cha Bibi Rukia (SA) kilicho mjini Qum Iran ametoa habari ya kuanzishwa tovuti ya wasomaji Qur'ani wa eneo la Sharqiyya ambalo ni eneo la wakaazi wengi wa Kishia nchini Saudi Arabia.
Ujumbe wa kituo hicho ukiongozwa na al-Makrani mwenyewe umeelekea nchini Saudia kwa shabaha ya kuvitembelea vituo vya Qur'ani katika miji ya Kishia ya Seihat, as-Sharqiyya na Qatif ambapo umeonana na kubadilishana mawazo na wasimamizi wa vituo hivyo kuhusiana na shughuli mbalimbali za Qur'ani Tukufu.
Katika safari hiyo al-Makrani ametoa mapendekezo kadhaa kwa wasimamizi wa vituo alivyotembela ikiwa ni pamoja na kushirikiana vituo hivyo katika kubadilishana uzoefu na walimu, kuanzishwa tovuti za wasomaji Qur'ani wanaotoka katika maeneo ya Kishia nchini Saudia na kuandaliwa mafunzo maalumu ya pamoja kwa madhumuni ya kulea na kufunza walimu wa Qur'ani.
Al-Makrani amesema kuwa kituo chake kiko tayari kutoa uzoefu na kubadilishana walimu kwa manufaa ya vituo hivyo vya shughuli za Qur'ani. 630373