Naibu Waziri katika wizara hiyo anayehusika na na masuala ya misikiti Walid Shuaib amesema akthari ya misikiti hiyo imejengwa kwa misaada ya wananchi.
Kwa mujibu wa gazeti la Kuwait Times, amesema nchini Kuwait kuna misikiti 1300 na kwa kuzingatia kuwa kila msikiti unahitajia Imamu na Muadhini, wizara hiyo inawategemea waadhini na maimamu kutoka nchi zingine za Kiislamu.
Walid Shuaib amesema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Wizara ya Waqfu ya Kuwait hualika makari kutoka nchi mbali mbali za Kiislamu ili wasome Quran katika misiktii mbali mbali ya Kuwait.
631126