Kwa mujibu wa gazeti la Sabah la nchini Uturuki, televisheni hiyo imekuwa ikichukua nyakati hizo kila siku kutoka kwa Baraza la Waislamu la Ujerumani na kisha kuwatangazia watazamaji wake.
Huku akiashiria kwamba televisheni hiyo inapasa kuwanufaisha wafuasi wa dini zote nchini Ujerumani, Carsten Molis mmoja wa wasimamizi wa televisheni ya RTL II amesema kwamba kama ambavyo vipindi mbalimbali maalumu vya Kikristo hutangaziwa wafuasi wa Ukristo kupitia televisheni hiyo katika siku za Krismasi, vipindi maalumu vya Kiislamu pia vinapaswa kutangaziwa Waislamu hasa katika mwezi huu wa Ramadhani ambao unaheshimiwa sana na wafuasi wa Uislamu.
Amesema hatua hiyo ni chanya katika kuleta usawa kati ya wananchi wote wa Ujerumani na kwa lengo la kuimarisha amani na utulivu miongoni mwa wafuasi wa dini mbalimbali nchini humo. 632194