Ratiba hizo ambazo zinajumuisha adabu na maadili ya Kiislamu katika mwezi huu mtukufu zilianza kutekelezwa Alkhamisi tarehe 12 Agosti, ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa baadhi ya nchi, na zitaendelea hadi tarehe 15 ya Ramadhani ambayo ni sawa na tarehe 26 Agosti.
Wahadhiri na wataalamu watakaohudhiria vikao hivyo ambavyo vitakuwa vikifanyika katika kituo hicho cha Kiislamu kabla ya futari, watakuwa wakijibu maswali mbalimbali ya washiriki yakiwemo ya saumu, mwezi wa Ramadhani na masuala mengine ya Kiislamu. Faida za funga katika mtazamo wa tiba na nafasi ya maadili katika utekelezaji wa sheria ni miongoni mwa maudhui muhimu zilizopangwa kujadiliwa katika vikao maalumu vya kituo hicho katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Ratiba nyingine muhimu ya kituo hicho katika kipindi cha siku 15 za mwanzo za mwezi huu ni sherehe maalumu za kusherehekea uzawa wa Imam Hassan Mujtaba (AS). 632213