Muungano wa Jumuiya za Kiislamu nchini Ufaransa umetoa wito kwa jumuiya za Kiislamu, misikiti na Waislamu wa nchi hiyo kutoa misaada yao kwa wananchi wa Pakistan wanaokabiliwa na janga kubwa la mafuriko.
Muungano huo umewataka Waislamu wa nchi hiyo kuchanga na kukusanya misaada ya kibinadamu inayotolewa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na kuipeleka kwa Waislamu wenzao wa Pakistan wanaokabiliwa na hali ngumu kutokana na mafuriko makubwa ambayo hadi sasa yameua maelfu ya watu na kuharibu nyumba za mamilioni ya wengine.
Katika sehemu nyingine ya wito huo, muungano huo wa jumuiya za Kiislamu umewashukuru viongozi wa Ufaransa kwa msaada wao kwa wananchi wa Pakistan na kuelezea matumaini yake kwamba misaada hiyo itaongezwa na kutolewa kwa wananchi waathirika hao kwa kiwango kikubwa zaidi. 633712