IQNA

Nchi za Kiislamu zapaswa kuwa na mpango wa kukabiliana na Utawala wa Kizayuni

11:23 - August 22, 2010
Habari ID: 1978166
Kunapaswa kuwa na mpango kamili wa kujihami iwapo Utawala wa Kizayuni wa Israel utathubutu kuishambulia nchi ya Kiislamu na hilo linaweza kufanyika tu kwa kuwepo mkataba wa usalama wa pamoja wa nchi zote za Kiislamu duniani.
Hayo yamesemwa na Muhammad Ali Romin Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu nchini Iran. Akizungmza katika kikao na waandishi habari kuhusu maadhimisho yajayo ya mwaka wa 31 wa Siku ya Kimataifa ya Quds, Romin amesema ‘hii leo ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na vita pamoja na hujuma vya vyombo vya habari vya Wazayuni na madola ya kibeberu’. Romin ambaye pia anasimamia masuala ya vyombo vya habari katika Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu amesema wanahabari Waislamu ni makamanda, maafisa na askari walio mstari wa mbele katika vita vya vyombo vya habari duniani na kwamba wana jukumu la kuweka wazi ukweli na kufichua njama zinazofanywa dhidi ya wanaadamu. Waziri huyo amesema suala la kususia bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel linapaswa kupewa kipaumbele na vyombo vya habari vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kuwazindua walimwengu.
Ali Romin Naibu Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu nchini Iran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukitoa vitisho dhidi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa zaidi ya miaka 31 sasa. Ameongeza kuwa mataifa mengine ya Kiislamu pia yanakabiliwa na tishio la utawala wa Kizayuni na kwa hivyo kuna haja ya nchi za Kiislamu kuwa na mkataba wa pamoja wa usalama ili kukabiliana na tishio la utawala wa Kizayuni.
Itakumbukwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds huadhimishwa kila mwaka katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika siku hiyo Waislamu na wapenda haki kote duniani hujitokeza katika maandamano ya kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel na kutangaza mfungamano wao na taifa linalodhulumiwa na Wazayuni la Palestina.
638313
captcha